
Morocco amesema kujitoa kwa Chad kumewaathiri kwani walikuwa manamatarajio makubwa zaidi kutokana na Pointi nne walizokuwa nazo mara baada ya kuichapa Chad bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Machi 23 Uwanja wa Ommisports Idriss Mahamat Ouya jijini ND’jamena.
Morocco amesema, wachezaji wanatakiwa kujiandaa zaidi na kujituma kwani mechi mbili ndio zilizobakia ambazo ni zamarudiano moja ikiwa ni dhidi ya Misri itakayopigwa Juni mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na ya pili ni dhidi ya Nigeria itakayopigwa ugenini Septemba mwaka huu.
Morocco amesema bado wanaamini nafasi ipo iwapo wachezaji watajiandaa vya kutosha kwa ajili ya michezo hiyo.
Chad ilikuwa kundi moja na Misri, Nigeria pamoja na Taifa Stars ambapo mara baada ya kujiondoa kuwania kucheza Afcon kila timu italazimika kudondosha pointi tatu kutoka katika Kundi G iliyopo Stars.
Hivyo, Stars iliyokuwa na pointi 4 imebaki na pointi moja tu, Nigeria itabaki na pointi mbili huku Misri ikibaki kileleni na pointi 4.
Mara baada ya Chad kujiondoa katika michuano hiyo, Shirikisho la Soka Barani Africa Caf lilimetangaza kuiondoa Chad katika michuano ijayo kuwania kufuzu kucheza Afcon na mingine yote iliyo chini yake huku ikitangaza kuitwanga Chad faini ya dolla 20,000 zaidi ya Sh milioni 44 kutokana na kitendo chake cha kujiondoa katika michuano ya ya kuwania kucheza Afcon.