
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, ligi hiyo yenye timu 12 itachezwa kwa mtindo uleule uliopangwa huku usajili kwa vilabu ukibaki vilevile kutokana na rufaa zote zilizokatwa kupitiwa na kukutwa hazina hoja za kutosheleza.
Alfred amesema, timu za mikoani zinazotarajiwa kuzindua michuano hiyo ni Baobao ikicheza dhidi ya Kagera Queens huku Sister ikicheza dhidi ya Panama.