
Kocha mtarajiwa wa Barcelona, Ronald Koeman akiwa katika majukumu yake ya kazi.
Rais wa Klabu hiyo, Josep Maria Baromeu ndiye aliyewathibitishia wanamichezo kuwa Koeman atatangazwa kuwa kocha wao siku chache zijazo na hii ni baada ya taarifa za kuondolewa kwa aliyekua kurugenzi wa ufundi , Eric Abidal.
FC Barcelona kwa sasa inatafuta Kocha mpya baada ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Kocha mkuu wa kikosi hicho kocha Quique Setién.
Uongozi w Barcelona umeamua kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya katika hatua ya robo fainali na Bayern Munich kwa Kipigo cha aibu cha mabao 8 - 2.
KWA NINI KOEMAN?
Barcelona wanatafuta kocha anayejua vizuri utamaduni wa klabu hiyo na Koeman anatajwa kuwa ni mtu sahihi kwa mahitaji ya mabingwa hao wa Ulaya mara tano kwa sababu amewahi kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 6 kati ya mwaka 1989 hadi 1995.
Pia Koeman aliwahi kufanya kazi kama Kocha msaidizi katika timu hiyo chini ya Kocha Louis van Gaal mwaka 1998 hadi 2000.
Kwa sasa FC Barcelona wapo kwenye mazungumzo na Shirikisho la soka Uholanzi KNVB ili kuhakikisha wanaipata huduma ya Kocha huyo.
Mkataba wa Koeman na FA ya Uholanzi unakipengele ambacho kimeainisha kuwa kama atahitajika na FC Barcelona basi ataruhusiwa kuondoka ingawa alisistiza kuwa yeye aanaweza kuachana na kikosi cha The Orange baada ya fainali za Euro mwakani 2021.
Makocha wengine waliokua wakihusishwa kujiunga na Fc Barcelona ni Mauricio Pochettino, Pep Guardiola na Xavi Hernandez.