Jumanne , 26th Oct , 2021

Kevin Durrant wa Brooklyn Nets ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 26 kufikisha alama 24, 007 kwenye historia ya NBA baada ya kukusanya alama 25, rebound 8 na Assits 4 zilizoisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa alama 104-90 dhidi ya Washington Wizard alfajiri ya leo Oktoba 26, 2021.

(Kevin Durrant akirusha mpira mbele ya mlinzi wa Washington Wizard alfajiri ya leo.)

Kwa alama hzizo 24, 007, Durrant anashika nafasi ya tatu kwa wachezaji wenye alama nyingi kwa wale wanaoendelea kucheza mpaka hivi sasa nyuma ya, Carmelo Anthony mwenye alama 27, 423 na kinara Lebron James wawili hawa wa LA Lakers huku James akiwa na alama 35, 445.

Durrant sasa ana saka alama 361 kuifikia nafasi ya 25 ya Gwiji wa zamani wa Philadelphia 76ers, Allen Iverson mwenye alama 24, 368.