Jumanne , 4th Aug , 2020

Timu ya Los Angeles Lakers imefanikiwa kumaliza kinara katika ukanda wa Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 baada ya kuifunga Utah Jazz kwa alama 116 kwa 108.

Nyota wa LA Lakers, LeBron James (Pichani) akionyesha ubora wake katika mechi ya NBA.

 

Mchezo huo ulifanyika katika Jiji la Florida Orlando huku nyota wa mchezo huo akiwa ni Antony David aliyefunga alama 42 huku Lebron James akichagiza ushindi huo kwa kutoa pasi za magoli 9 na kufunga alama 22.

Katika michezo mingine iliyochezwa siku ya Jumatatu, New Orleans Pelicans waliifunga Memphis Grizzlies kwa alama 109-99 ,wakati mabingwa watetezi Toronto Raptors waliibuka na ushindi wa alama 107 dhidi ya 103 za Miami Heat.

Denver Nuggets walihitaji muda wa ziada kuifunga Oklahoma City Thunder kwa alama 121 kwa 113,na walimaliza katika nafasi ya tatu kwa ukanda wa Magharibi nyuma ya Los Angeles Clippers nayo Indiana Pacers ikainyuka 111 kwa 100 na kushika nafasi ya tano ukanda wa Mashariki.