Jumatatu , 12th Oct , 2020

Nyota wa Los Angeles Lakers, LeBron James ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza katika ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani kutwaa tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi katika fainali ya michuano hiyo akiwa na timu tatu tofauti.

Nyota wa Los Angeles Lakers, LeBron James akiwa na tuzo alizotwaa baada ya kuisaidia timu yake kutwaa NBA.

LeBron alitwaa tuzo ya MVP akiwa na Miami Heat mwaka 2012 na 2013, pia alitwaa akiwa na Cleveland Cavaliers mwaka 2016 na leo aliisaidia Lakers kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 baada ya kuinyuka Miami Heat kwa alama 106-93 uliopelekea kushinda katika michezo 4-2.

Wachezaji pekee waliowahi kutwaa tuzo hiyo kwa zaidi na timu moja ni pamoja na Kareem Abdul-Jabbar (Milwaukee Bucks na Los Angels Lakers), na Kahwi Leonard (San Antonio Spurs na Toronto Raptors).

Katika ushindi huyo LeBron aliondoka katika mchezo akipata Triple Double ikiwa na maana ya kufunga pointi 28, mipira ya kurudi 11 na pasi ya usaidizi 10 katika mchezo huo.

Ushindi huo pia umewafanya Lakers kufikia rekodi ya Boston Celtics ya kutwaa mataji mengi ya NBA ambayo ni mara 17.