Alhamisi , 6th Aug , 2020

Meneja wa mshambuliaji wa Simba sc Meddie Kagere ajulikanaye Kama Patrick Gakumba amesema mchezaji wake tayari ameongeza mkataba wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa nchi.

Mshambuliaji wa klabu ya Simba,Meddie Kagere akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi.

Gakumba amesema Kagere amerefusha mkataba kwa mwaka mmoja mwingine utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2021 baada ya mkataba wake wa mwanzo kusaliwa na mwaka mmoja .

Kagere ambaye ni mfungaji Bora wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo alijiunga na Simba sc katika msimu wa mwaka 2018 akitokea Gormahia ya Kenya.

Ziliibuka tetesi kuwa klabu ya Levante ya Hispania ilikua ikiwania saini ya mshambuliaji huyo ingawa wakala Gakumba alisema waliipa nafasi ya kwanza Simba kutokana na mwekezaji katika timu hiyo Mohamed Dewji hataki kuruhusu wachezaji bora kuondoka katika kikosi cha Simba.

Nyota huyo wa Kimataifa wa Rwanda amekua na mchango mkubwa kwa wekundu wa msimbazi Simba kwani katika misimu yake miwili ameifungia mabao 45 katika misimu yake miwili ya ligi kuu Tanzania Bara.