Alhamisi , 6th Aug , 2020

Kocha mkuu wa Mbao FC ya jijini Mwanza, Fred Felix Minziro amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20.

Kocha Fred Felix Minziro

Minziro amewashinda Aristica Cioaba wa Azam na Amri Said wa Mbeya City, akishinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Mbao FC kushinda michezo mitano kati ya sita waliyocheza ndani ya mwezi Julai na kupata sare moja.

Kwa sasa kocha Minziro na kikosi cha timu ya Mbao wapo Ligi daraja la Kwanza FDL mara baada ya kutoka suluhu ya 4-4 dhidi ya wawakilishi wa jiji la Mbeya Ihefu FC katika mchezo wa mtoano playoff ya kinyang'anyiro cha kukata tiketi ya ushiriki Ligi Kuu Tanzania bara VPL, ambapo Ihefu walifaidika na goli la ugenini.

Wakati huohuo mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Waziri Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20, Waziri amewashinda Peter Mapunda wa Mbeya City na Obrey Chirwa wa Azam FC alioingia nao fainali.