Ijumaa , 15th Jan , 2016

Ligi Daraja la Kwanza inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku timu 3 za juu ambao ni vinara kutoka katika kila kundi zikipata nafasi ya kupanda ligi kuu msimu ujao.

Kundi A, Jumamosi Mji Mkuu watawakabili Africa Lyon uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, KMC dhidi ya Kiluvya uwanja wa Mabatini Mlandizi, Polisi Dodoma watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Mgambo Mpwapwa, huku Jumapili Polisi Dar wakiwakaribisha Ashanti uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Kundi B, Njombe Mji watakuwa wenyeji wa Kimondo uwanja wa Amani Njombe, Lipuli FC dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi – Mafinga, uwanja wa Majimaji mjini Songea JKT Mlale watakuwa wenyeji wa Polisi Morogoro, huku Jumapili kukichezwa mchezo mmoja Ruvu Shooting dhidi ya Burkinafaso uwanja wa Mabatini, Mlandizi.

Kundi C, Rhino Rangers watawakaribisha JKT Kanembwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Panone FC dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ushirika mjini Moshi, uwanja wa Karume Musoma, wenyeji Polisi Mara watacheza dhidi ya Polisi Tabora, huku siku ya Jumapili Mbao FC wakiwakaribisha JKT Oljoro uwanja wa CCM Kirumba.