 
Ni kwa mara ya kwanza KMC wanakutana na Dodoma jiji FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara
Ni kwa mara ya kwanza timu hizi zinakutana katika michezo ya ligi kuu, hivyo huu ni mchezo wa kihistoria kwa timu hizi mbili, kwani huu ni msimu wa kwanza kwa Dodoma jiji kucheza ligi kuu wakati KMC huu ni msimu wao wa tatu.
Timu hizi zinatofautiana alama 2 tu, kwenye msimamo wa ligi, KMC wapo juu katika nafasi ya 8, wakiwa na alama 18, wakati Dodoma wapo nafasi ya 9 na alama 16.
Wenyeji KMC wanaingia uwanjani wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, katika michezo yao mitatu ya mwisho, wameshinda mara mbili dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0 na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Gwambina na sare mchezo 1 dhidi ya Biashara United sare ya bao 1-1.
Wakati Dodoma jiji FC wameshinda mchezo mmoja tu kwenye michezo 3 ya mwisho, wameshinda dhidi ya Ihefu ushindi wa bao 3-0, walipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara na walifungwa 3-0 na Azam FC.
Mchezo huu unachezwa Saa 10:00 Jioni uwanja wa Uhuru.
Michezo mingine ya raundi ya 14 itakayochezwa wikiendi hii ni,
Jumamosi Disemba 05, 2020
Coastal Union Vs Mbeya City
	Tanzania Prisons Vs Kagera Sugar FC
	 
Jumapili Disemmba 06, 2020
	Mtibwa Sugar Vs Mwadui FC
	Ihefu SC Vs JKT Tanzania
	Yanga SC Vs Ruvu Shooting
	 
Jumatatu Disemba 07, 2020
	Gwambina Vs Azam FC
	 
Jumatano Disemba 09, 2020
	Simba VS Polisi Tanzania
	Namungo Vs Biashara United

 
 

 
 
 
 
 
