Michuano hiyo ilianza mwanzoni mwa Mei mwaka huu lakini ilisimama baada ya viwanja vya Gymkhana, Leaders na Burhani cha Upanga kujaa maji kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hapa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa ufundi wa Chama cha Karate nchini TKF, Hamis Hassan amesema michuano hiyo itaanza kwa kuchezwa katika uwanja wa Leaders kati ya timu ya Union watakaocheza na Veecom B wakati Veecom A wakichuana na Moro huku Burhani wao wakipepetana na Telugu.
Katika uwanja wa Burhani timu ya Dik Diks itachuana vikali na Estim wakati St Gobian itaumana na GP na Upanga itacheza na AKSC.