
Nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya JKT Tanzania, Baraka Sadick akionyesha ufundi wake.
Mchezo wa mapema hii leo utapigwa majira ya saa 12 jioni ukizikutanisha mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Vijana City Bulls dhidi ya Ukonga Kings.
Mchezo mwingine utachezwa katika uwanja wa Don Bosco saa 2 usiku ukizikutanisha Pazi dhidi ya Panthers.
NBL ilianza kutimua vumbi Oktoba 18 mwaka huu ikihusisha timu 10 ambapo kwa jiji la Dar es salaam limetoa timu 7 na mikoani timu 3.
Bingwa wa NBL ataiwakilisha nchi kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika wakati mshindi wa pili na wa tatu watacheza mashindano ya kanda ya tano (Zote 5).
Kundi A lina timu tatu ambazo ni JKT, Oilers na Kurasini Heat, kundi B linatimu za Savio, ABC, Rukwa Stars na Korogwe Heat, kundi C linajumuisha Vojana City Bulls, Ukonga Kings, Pazi na Don Bosco Panthers .
Upande wa wanawake zipo timu tano ambazo ni Don Bosco Lioness, Dodoma Queens, Jeshi Stars, JKT Stars na Vijana Queens.
Ligi hiyo inatarajiwa kufikia tamati Oktoba 25 mwaka huu ambapo mabingwa watajulikana.