Alhamisi , 28th Apr , 2022

Klabu ya liverpool sasa haijapoteza mchezo katika uwanja wa Anfield kwenye michezo 12 ya hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya wakishinda michezo 10 na kutoka sare 2 baada ya kuwalaza Villareal magoli 2 kwa 0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya pili

(Wachezaji wa Liverpool Sadio Mane na Luis Diaz)

Na nyota wa klabu hiyo Sadio Mane sasa amekua mchezaji wa pili kutoka Africa aliyefunga magoli mengi zaidi katika hatua za mtoano za ligi ya mabingwa barani Ulaya akifikisha magoli 14 sawa na Didier Drogba. Pia idadi hiyo ya magoli imemfanya Sadio Mane kua mchezaji wa pili aliyefunga magoli mengi zaidi katika hatua hiyo ya ligi ya mabingwa tangu msimu wa mwaka 2017/18 akizidiwa na Karim B enzema aliyefunga magoli 16.

(Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp)

Vile vile kalbu ya Liverpool wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kumpa kandarasi mpya kocha wao Jurgen Klopp baada ya Mjerumani huyo kuonesha nia ya kuwa tayari kuongeza muda wake wa kuendelea kusalia katika viunga vya anfield.

Nia ya Klopp ilikua ni kuondoka kuondoka LIverpool wakati mkabata wake wa sasa utakapomalizika majira ya joto msimu wa mwaka 2024 na mara kadhaa alikua akisisitiza kwamba ataondoka klabu hapo baada ya mkaba wake kumalizika mwaka 2024, lakini sasa imeonyesha nia ya kufungua milango ya mazungumzo kwa ajili ya kuongeza muda wa mkataba huo.

Lakini Klopp ameongezewa nguvu msimu huu na wamiliki wa Liverpool, wanafahamu hili vyema na watafanya kila wawezalo kufikia makubaliano ya kumbakisha Klopp kuendeloea kukino akikosi hicho cha majongoo wa Anfield.