Alhamisi , 3rd Dec , 2020

Kocha mpya wa klabu ya Azam, George Lwandamina amesema yupo tayari kwa changamoto mpya katika ligi kuu Tanzania bara ambayo kwa asilimia kubwa ina ushindani wa hali ya juu.

Kocha mpya wa Azam, George Lwandamina, (Kulia) alipokua anaifundisha Yanga akisaidiwa na Juma Mwambusi (kushoto).

Lwandamina ambaye aliwasili usiku wa kuamkia leo, amesema anaifahamu ligi ya Tanzania bara, na uzoefu wake kufanya kazi Yanga inatosha kumpa mwanga wa kujua wapi pa kuanzia.

''Kazi ya ukocha sikuzote ni ya changamoto, nimekuja Azam na najua wanahitaji nini, tutajadili kwa pamoja juu ya namna ya kufikia malengo yaliyowekwa, nadhani tutafanikiwa kwakuwa ninauzoefu wa ligi ya hapa'' alisema Lwandamina.

Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu wa Azam Fc, Abdulkarim Amim Popat amesema waliamua kumchagua Lwandamina kutokana na wasifu wake katika soka la Tanzania haswa ikichagizwa na kuifundisha Yanga na kuipa ubingwa katika wakati wake.

Vilevile , Popat ameongeza kwamba wameamua kufanya kazi na Lwandamina kwa msimu huu pekee na hapo baadae watajadili zaidi juu ya kurefusha mkataba kulingana na makubaliano ya awali.