Harry Maguire akiwa na golikipa wa timu ya taifa ya England Jordan Pickford
Kwa sasa Maguire yupo na kikosi cha timu ya taifa ya England kwenye michuano ya Euro 2020 na watashuka dimbani leo Usiku Saa 4:00 kucheza dhidi ya Denmark kwenye mchezo wa nusu fainali. Beki huyo ameonyesha kiwango bora mpaka sasa kwenye michuano hiyo akiwa amefunga bao moja na alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kwenye mchezo wa 16 bora dhidi ya Ujermani.
Kuelekea mchezo wa usiku wa leo Vidic alipata nafasi ya kuzungumzi kiwango cha Harry Maguire,
“Harry Maguire anaonekana kujiamini na mtulivu zaidi akiwa na timu ya taifa kuliko akiwa na Manchester United. Yeye ni mlinzi ambaye bado anaendelea kuimarika, lakini kama anataka kutambulika kwa kiwango cha juu lazima atwae mataji. Ninapomtazama Maguire naona mlinzi ambaye yupo vizuri kwenye kila kitu. Yeye sio mzuri kwenye mpira au kasi kama vile Rio Ferdinand, Lakini ana ubora namna anavyocheza. Ana kasi ya kutosha, ana nguvu za kutosha, anaweza kuruka na kucheza mipira ya juu, lakini pia anauwezo wa kukaa kwenye nafasi.” Amesema Nemanja Vidic
Maguire amekuwa kwenye ukosoaji mubwa kutoka kwa wadau mbali mbali kutokana na kiwango chake tangu ajiunge na Manchester United akitokea Leicester City kwa ada ya uhamisho ya pauni million 80 mwaka 2019 ambayo ni zaidi ya billion 256 kwa pesa za kitanzania.
Vidic alicheza Manchester United kuanzia mwaka 2004 hadi 2014 na alitwaa jumla ya mataji 15 ukiwemo ubingwa wa Ligi Kuu England mara tano na ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara moja, katika michezo 300 na alifunga jumla ya mabao 21.




.jpg?itok=0CrdpE0P)
