Jumatano , 28th Nov , 2018

Mlinda mlango mkongwe nchini Juma Kaseja, amesema ni kosa kubwa wanalofanya mashabiki wa soka nchini ni kumfananisha yeye na golikipa namba moja wa Simba Aishi Manula.

Manula kushoo na Juma Kaseja

''Kiukweli kutufananisha mimi na Aishi ni kosa kwasababu kila mtu ana uwezo wake na kikubwa zaidi mimi nimeanza na nimecheza kwa kiwango kikubwa tu'', Kaseja ameiambia www.eatv.tv

Kwa upande mwingine Kaseja bado ana kiwango kikubwa cha kucheza lakini ni wakati wa Aishi Manula kupata nafasi kwenye timu ya taifa lakini hiyo haimnyimi yeye nafasi ya kucheza timu nyingine ndio maana ameitwa timu ya taifa ya soka la ufukweni.

Siwezi kumwongelea sana Manula ana uchezaji wake na mimi nina aina yangu ya kucheza hivyo hatufanani na siwezi kumwongelea sana kwasasa labda nikistaafu nikawa mtazamani kama mashabiki wengine ninaweza kuwa na nafasi ya kuongelea zaidi uwezo wake.

Kaseja amekuwa golikipa mwenye mwendelezo mzuri tangu alipoanza kucheza soka ngazi za vilabu akiitumikia Moro United na baadae Simba,Yanga, Kagera Sugar na sasa KMC.