
Picha kunogesha logo ya michuano ya UEFA EUROPA ligi msimu mpya wa mwaka 2021-2022.
Westham imepangwa kwenye kundi hilo mchana wa leo Agosti 27, 2021 katika hafla fupi ya kuchezesha droo ya upangaji makundi ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye mji wa Istanbul nchini Uturuki na mchezo wa fainali wa kutamatisha michuano hiyo utachezwa kwenye uwanja wa Roman Sanchez Pzjuan nchini Hispania disemba 9, mwaka 2022.
Leicester City imepangwa kwenye kundi C kucheza dhidi ya Napoli ya Italia, Spartak Moscow kutoka Urusi pamoja na Legia Warsaw ya nchini Poland ilhali kundi E likitazamiwa kuwa kundi la kifo kwa kuwajumuisha Lazio ya Italia, Lokomotiv Moscow kutoka Urusi na Galatasaray inayowakilisha nchi ya Uturuki.
Kwenye makundi mengine, Lyon (Ufaransa), Rangers (Scotland), Sparta Prague (Jamhuri ya Czech) na Brondby (Denmark), kundi B, AS Monaco (Ufaransa), PSV Eindhoven (Uholanzi), Real Sociedad (Hispania), Sturm Graz (Austria), kundi D, Olympiakos (Ugiriki), Eintracht Frankfurt (Ujerumani), Fenerbanhce (Uturuki), Royal Antwerp (Belgian).
Kundi F, Braga (Ureno), Red Star Belgrade (Serbia), Ludogorets (Bulgaria), Midtjylland (Denmark) na kundi G, Bayer Leverkusen (Ujerumani), Celtic (Scotland), Real Betis (Hispania), Ferencvaros (Hungary).
Na kwa upande mwingine;
Mshambuliaji wa Villareal Gerrard Moreno amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Europa ligi baada ya kuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 7 na ku-assist 5 na hatimaye kuwapiku kiungo mshambuliaji, Bruno Fernandez na Edinson Cavani wote kutoka Manchester United.
(Mshambuliaji wa Villareal, Gerard Moreno akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Manchester United kwenye fainali ya EUROPA ligi.)
Mabao na assist za Moreno zimeisaidia 'Nyambizi ya Hispania', Villareal kubeba kombe la michuano hiyo msimu wa mwkaka 20210-2022 ikiwa ni kwa mara ya kwanza.