Alhamisi , 20th Aug , 2020

Msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England EPL utaanza kutimua vumbi jumamaosi ya Septembe 12 mwaka 2020 ikiwa ni wiki sita tu zimepita tangu kumalizika kwa msimu wa 2019-20 na utamalizika mei 23 mwaka 2021.

Kiungo matata wa Manchester United, Bruno Fernandes (pichani) anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika EPL msimu ujao.

Jumla ya timu 20 zitaminyana kuwania ubingwa wa ligi hiyo tajiri Duniani, Liverpool ndio mabingwa watetezi na watakuwa na kibarua cha kuutetea ubingwa huo walioutwaa msimu uliopita kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 30.

Timu zilizopanda daraja msimu huu ni Leeds United ,West Bromwich Albion na Fulham zote hizi zimechukua nafasi za timu zilizoshuka daraja ambazo ni AFC  Bournemouth, Watford na Norwich City.

Kwa mujibu wa ratiba Derby ya jiji la Manchester Manchester Derby kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City mchezo wa kwanza Man United watakuwa wenyeji wa Man City katika Dimba la Old Trafford Desemba 12 na mchezo wa pili utachezwa Marchi 06 katika dimba la Etihad.

Ratiba ya Michezo mingine ya Derby ni kama ifuatavyo.

Derby ya jiji la Liverpol kati ya Everton na Liverpool ‘Merseyside derby’

• October 17 2020 Everton v Liverpool
• February 20 2021 Liverpool v Everton

Derby kati ya Manchester United na Liverpool ‘North West derby’
• January 16 2021 Liverpool v Manchester United
• May 05 2021 Manchester United v Liverpool

Derby ya Kaskazini mwa jiji la London Kati ya Arsenal na Tottenham ‘North London’ derby
• Tottenham v Arsenal - Dec 5
• Arsenal v Tottenham - Mar 13

Derby ya Maghalibi mwa jiji la London kati ya Fulham na Chelsea ‘West London derby’
• Fulham v Chelsea - Jan 16
• Chelsea v Fulham - May 1

Wiki ya kwanza ya EPL itachezwa michezo nane tu,michezo sita itachezwa jumamosi September 12 na September 14 itachezwa michezo miwili.

Klabu za Manchester United na Manchester city hazitacheza wiki ya kwanza kutokana na ushiriki wao wa michuano ya vilabu barani ulaya hivyo zilipewa siku 30 za mapumziko.

Ratiba wiki ya kwanza ya Ligi kuu England EPL
Jumamosi 12 September
• Crystal Palace V Southampton
• Fulham V Arsenal
• Liverpool V Leeds United
• Spurs V Everton
• West Brom V Leicester City
• West Ham V Newcastle United

Jumatatu 14 September
• 20:00 Brighton V Chelsea
• 20:00 Sheffield United V Wolves