
Florian Wirtz - Nyota wa Bayer Leverkusen
Sababu za msingi kwa Man City kujiondoa ni gharama kubwa zilizotajwa kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 22. Wirtz, ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kikosi cha Leverkusen msimu uliopita, alionekana kama mrithi wa Kevin De Bruyne anayeondoka Man City.
Magoli 18 na asisti 20 yalimfanya chipukizi huyo kutambulika kimataifa msimu uliopita, na msimu huu amefunga mabao 16. Kikosi cha Pep Guardiola si mara ya kwanza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwanunua wachezaji wenye gharama kubwa ikiwemo Harry Kane wakati Daniel Levy ada ya pauni milioni 150 na badala yake wakalipa pauni milioni 100 kwa Jack Grealish na pauni milioni 51 Erling Haaland.