Jumanne , 21st Mar , 2017

Manchester City imeshitakiwa na chama cha soka nchini Uingereza, FA kwa kitendo cha wachezaji wake kuonesha utovu wa nidhamu kwenye mechi dhidi ya Liverpool Jumapili iliyopita.

Wachezaji wa Man City wakizonga mwamuzi

Tukio lililoiponza City, ni pale wachezaji wake walipomzonga mwamuzi Michael Oliver kunako dakika ya 50, kupinga penati iliyopewa Liverpool, kufuatia mlinzi wao Gael Clichy kumkwatua Roberto Firmino.

Liverpoo walifunga penati hiyo, iliyopigwa na James Milner, na kufanya kuongoza, bao moja kwa bila, kabla ya baadae City, kufunga bao la kusawazisha kupitia Sergio Aguero.

Man City, wamepewa hadi Alhamisi saa 2:00 usiku kuwa tayari kujibu mashtaka hayo.