Manara ashusha lawama kwa wachezaji

Jumapili , 5th Jan , 2020

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amevunja ukimya na kufunguka kilichoiadhibu klabu yake katika mchezo wa ligi dhidi ya watani wao Yanga.

Haji Manara

Manara amesema kuwa Simba ilistahili kushinda mchezo huo kutokana na uwekezaji ambao umefanywa mpaka sasa, huku akiwarushia lawama baadhi ya wachezaji kwa kutocheza kama mashabiki walivyotegemea.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2, Simba ikitawala kwa kipindi cha kwanza ambapo ilipata bao moja, huku Yanga ikiamka na kushambulia kwa nguvu katikati ya kipindi cha pili na kufanikiwa kurejesha mabao yote mawili.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Lau wachezaji wetu mngekumbuka maneno ya huyu Tajiri siku ya mchezo wa jana, hz tambo za kupata droo zisingekuwepo!! Wenzenu hawapati mnachokipata,,wanapanda daladala hadi Mbeya,hawakai camp nzuri,hawalipwi kwa wakati,hawapati bonus mzipatazo lakini wanawazidi fighting spirit na commitment kwa mbali sana!! Bado thamani ya Jezi ya Simba kwa baadhi ya Wachezaji wetu mnaiangusha, kweli mpira una matokeo matatu ila kwa jana bila kupepesa macho ile sare haikustahili kwa ukubwa wa Simba, mmewaangusha sana Washabiki wetu ambao always wanakuja kuwapa nguvu,,mm binafsi najiuliza ntakuwa nayo legitimacy ya kuwaita kwa nguvu Washabiki uwanjani? Bodi yetu makini mmeiangusha, Management tumelowa kabisa , na mnampa wakati mgumu mno tajiri anaeweka pesa zake, kifupi baadhi yenu mmeboa mno!!!! ( ukweli mchungu)

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on

Sare hiyo imeonekana kufurahiwa na mashabiki wa Yanga huku wengi wakisema kuwa Simba walikwenda uwanjani na matokeo yao, hivyo wanafurahia kwa sababu walijihisi wanyonge kabla ya mchezo.