
Aliyekua Rais wa TFF , Jamali Malinzi enzi za utawala wake alipokua akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbali mbali ya mpira wa miguu.
Kauli ya Manara inakuja kufuatia Kamati hiyo kuchelewa kutoa maamuzi juu ya uhalali wa Mkataba wa winga Benard Morrison ambaye anatajwa kuwa alisaini kuitumikia Yanga kwa miaka miwili lakini nyota huyo anaukama mkataba huo.
Manara amemkataka Mwenyekiti wa Kamati hiyo Elias Manyala kutenda haki, kwani zama za ujanja ujanja zimefikia mwisho katika Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pom,be Magufuli ambaye hapendi ubabaishaji.
Ameongeza kuwa vyombo mbali mbali vya Serikali vinalifuatilia suala hili kwa umakini na iwapo kuna udanganyifu upo uwezekano baadhi ya Viongozi watawekwa jela kama ilivyokua kwa aliyekua Rais wa TFF wa awamu iliyopita, Jamali Malinzi.
Aidha Manara amedai kwamba haiwezekani Kamati ikaifuta hoja iliyoletwa na Mjumbe juu ya kesi ya kuchunguza iwapo Yanga ilighushi mkataba wa nyota huyo ambaye wiki iliyopita alitambulishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mali ya klabu ya Simba.