
(Kocha wa Manchester United Ralf Rangnick)
Kocha wa muda wa manchester united Ralf Rangnik amethibitisha kuwa atawakosa wachezaji wake sita ambao ni nahodha Harry Maguire, Jadon Sancho, Paul Pogba, Fred, Edinson Cavan, na Luke Shaw wanaoendelea kujiuguza majeraha, huku taarifa zikisema Harry Maugire anaweza kukosekana kipindi chote cha msimu kilichobaki kufuatia kuumia goti akiwa mazoezini.
Naye kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amethibitisha kuwakosa nyota wake wa nne ambao ni Ben Chilwell, Mateo Kovacic, Ross Barkley, na Callum Hudson-Odoi wanaosumbuliwa na majeraha. Chelsea wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu kutoakana na muendelezo wa matokeo yasiyoridhisha waliopata Manchester united katika michezo yao iliyopita.