Alhamisi , 2nd Dec , 2021

Chama cha mchezo wa tennis duniani upande wa wanawake wamezuia mashindano yote yaliyopaswa kufanyika nchini China mpaka sakata la unyanyasaji wa kijinsia la nyota kutoka   nchini humo  Peng Shuai kupatiwa ufumbuzi.

(Mcheza tennis wa China, Peng Shuai na ujumbe alioutuma online)

Peng 35, aliyewahi kushika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani kwa wachezaji wawili wawili kwenye tennis hakuonekana hadharani kwa siku 13 baada ya kuchapisha maneno kwenye mitandao yake ya kijamii mnamo November 2, 2021 kwamba aliyekuwa Waziri mkuu msaidizi nchini humo Zhang Gaoli alikuwa anamlazimisha kimapenzi kipindi alipokuwa hayupo kwenye mahusiano

Chapisho hilo lilikuja kufutwa saa chache baadae ingawaje tayari watu wengi walikuwa wamelisambaza na wasiwasi zaidi ukiongezeka kwa kutoonekana hadharani majuma mawili kwa nyota huyo

Mtendaji mkuu wa WTA, Steve Simon amesema “Bado tuna mashaka na usalama wa Peng, kama yupo huru, salama na kama hajatishiwa usalama wake” na kuendelea kusisitiza “kwa mazingira mazuri ya kiusalama , sidhani kama ninaweza kuwaambia wachezaji waende wakashindane huko”

 WTA kimetoa wito wa kuchunguzwa madai ya Peng huku wakisisitiza lazima ufanyike uchunguzi wa kina tena ulio wazi na huru bila ya kuwepo kwa vitisho.

Mara ya mwisho kuonekana kwa Peng ilikuwa mwisho wa mwezi Novemba 2021 kwenye michuano ya Beijing ya tennis kisha baadae kipande cha video kurushwa mtandaoni akiongea na rais wa kamati ya olimpiki (IOC) Thomas Bach na kusema yupo salama na mzima.

 Mamlaka za China zimesema suala la Peng  ni siasa za kimichezo tu.