Ijumaa , 15th Oct , 2021

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika ‘CAF’ limeruhusu mashabiki kwenye michezo yake ya kombe la shirikisho Afrika na Ligi ya mabingwa barani humo kwa timu za Tanzania inayotaraji kuchezwa kuanzia Ijumaa ya leo Oktoba 15,2021.

(Picha ikionesha Mashabiki wa Simba SC (kwenye picha kubwa), Mashabiki wa Azam (Juu kulia) na Kikosi cha timu ya Biashara United Mara)

Barua CAF iliyowasilishwa na TFF kwa Umma navilabu husika:

(Barua ya TFF yenye Ujumbe wa CAF)

Kwa Mujibu wa taarifa ya CAF iliyotolewa na TFF usiku wa jana Oktoba 14, 2021, mchezo wa shirikisho wa mzunguko wa pili hatua ya mtoano kati ya Biashara United Mara na Al Ahly Tripoli utakaochezwa saa 9:00 Alasiri kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam utaruhusiwa kuingiza mashabiki 5, 000.

Kwa upande mwingine, Mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika wa Azam dhidi ya Pyramids utakaochezwa kwenye dimba la Chamazi saa 9:00 Alasiri utaruhusiwa kuingiza mwatazamaji  2,000 ilhali Simba wameruhusiwa kuingiza mashabiki 15, 000 kwenye mchezo wake wa marudio utakaochezwa Oktoba 24, 2021