Alhamisi , 14th Oct , 2021

Kocha Msaidizi wa kikosi cha Simba, Mrwanda Hitimana Thierry amesema mchezaji mbadala wa kutengeneza nafasi za mabao klabuni hapo tayari ameshapatikana baada ya Chama kuondoka na wana matarajio makubwa kuwa atafanya vizuri.

Kocha Msaidizi wa Simba, Hitimana Thierry akiwa anasimami mazoezi.

Hitimana ameyasema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika ambapo Simba itacheza Jmapili 17, 2021 dhidi ya Jwaneng Galaxy nchini Botswana.

Hitimana amesema, “Katika hizi mechi ambazo tumecheza tumeona jinsi gani tulikuwa tukitengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia, lakini mtu wa kutengeneza nafasi ya mwisho, tayari yupo mtu ambaye amepewa jukumu hilo na kuna matarajio makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wetu huu"

Maelezo ya Hitimana hayakutaja kwa jina mchezaji huyo mwenye majukumu hayo mapya lakini ripoti za kikachero zinaripoti kuwa ni miongoni mwa kiungo fundi, Larry Bwalya, winga Bernanrd Morrison na Pape Ousmane Sakho. Ikumbukwe kuwa Chama alikuwa kinara wa kutengeneza nafasi za mabao 'Assits' wa Ligi kuu msimu ulioisha 2020-21 kwa kutengeneza nafasi 15 na hata msimu juzi 2019-20 alitoa assist 8 na kuwa kinara katika VPL.

Msimu uliopita Bwalya alikuwa na assist 5 na Bernard Morrison alikuwa na assist 4 licha ya kukosa utulivu na kuwa na ingia toka kwenye kikosi cha kwanza ilhali Sakho alikuwa mchezaji bora wa Lgi kuu ya Senegel.

Kwa upande mwingine amegusia mazingira ya nchini Botswana ambayo wanajiandaa kukabiliana nayo.

“Tumejiandaa vizuri kimbinu na kiufundi, pia tumeshajua tutaenda kucheza kwenye joto kali, tumeanza kulifanyia kazi hilo na kuzoea hali hiyo kabla ya kuondoka kuelekea Botswana". Amesema Hitimana.

Simba inataraji kuondoka nchini Tanzania Ijumaa ya 18, 2021 kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo huo.