Jumatatu , 6th Dec , 2021

Kuelekea Desemba 9, mwaka huu Azam ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar, kila upande umepania kuibuka na ushindi.

Idris Mbombo

Mshambuliaji wa Azam, Idriss Mbombo, amesema amejipanga kuwamaliza Kagera Sugar kwenye mchezo huo ili kuipa timu yake alama tatu.

Mbombo mwenye mabao mawili, amesema: “Nina hamu ya kuwafunga Kagera na kuipa
alama tatu timu yangu.“Nina imani mpaka ligi inamalizika ninaweza kuwa mfungaji bora maana timu yangu inanipa sapoti kubwa.”

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza, ameweka wazi kuwa: “Tumetoka kupoteza
mchezo ugenini dhidi ya Ruvu Shooting, kwa sasa tumejaribu kufanya mabadiliko makubwa na thabiti yenye ubora wa hali ya juu, tunaamini mchezo ujao dhidi ya Azam tutafanya vizuri.

“Kwa upande wa wachezaji, kikosi kipo tayari isipokuwa tuna majeruhi wawili ambao hawataweza kushiriki mchezo
huo, waliobaki wote wapo vizuri kiafya, niwatoe wasiwasi mashabiki zetu tumejiandaa vya kutosha kupata ushindi.”