AS Adema dhidi ya SO l'Emyrne
Kisa kilianza baada ya SO l'Emyrne kukasirishwa na maamuzi ya refa kwenye mechi yao iliyopita, yaliyowagharimu ubingwa. Hasira hiyo iliwafanya wachague njia ya ajabu kabisa kuonyesha malalamiko yao.
Badala ya kucheza kawaida, walianza kujifunga magoli mfululizo kuanzia dakika ya kwanza, Kila walipopata mpira, waliurudisha golini kwao bila hata kushambulia upande wa pili wakionesha wazi kupingana na mwamuzi wa mchezo.
Mashabiki walibaki wameshtuka, baadhi wakicheka, wengine wakiondoka uwanjani. Baada ya tukio hilo, wachezaji na makocha walichukuliwa hatua kali, lakini mechi hiyo iliingia kwenye historia kama moja ya matukio ya ajabu zaidi kuwahi kutokea kwenye soka









