Alhamisi , 9th Sep , 2021

Klabu ya Nice kutoka nchini Ufaransa wamepokwa pointi mbili na shirikisho la soka nchini humo, huku moja ikishikiliwa na Uongozi wa Ligi hiyo ambapo umeamuru kurudiwa kwa mchezo wao dhidi ya Olympique de Marseille ambao ulivurugika agosti 22 mwaka huu.

Taharuki kati ya wachezaji wa Marseille dhidi ya Mashabiki wa Nice iliyojitokeza Agosti 22 kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Ufaransa.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye huko Nice Allianz Riviera ilihudhuriwa na umati wa zaidi ya watu 32,000 huku watazamaji wakiruhusiwa kurudi ndani ya Uwanja huko Ufaransa baada ya msimu mwingi wa 2020-21 ulichezwa bila mashabiki kwa sababu ya vizuizi vya UVIKO-19.

Nice ilikuwa ikiongoza bao1-0 mpaka dakika ya 75 kabla ya mashabiki kuvamia uwanja na kupelekea Refa kuvunja mchezo huo baada ya Dimitri Payet wa Marseille kupigwa na chupa na mashabiki wa timu pinzani ambapo mchezaji huyo alishindwa kuvumilia na kupelekea kuokota chupa hiyo na kuitupa tena kwenye umati wa mashabiki wa Nice .

Ligue de Football Professionnel (LFP) ilitangaza maamuzi hayo ya kinidhamu Jana usiku na Payet kukumbana na kifungo cha mechi moja wakati wachezaji wengine wa Marseille waliokumbana na adhabu hiyo ni Alvaro Gonzalez ambaye amesimamishwa kwa mechi mbili wakati mkufunzi wa mazoezi wa Marseille, Pablo Fernandez amepewa adhabu ya kutokuwepo uwanjani kwa miezi tisa, hadi 30 Juni 2022.