Jumapili , 8th Jun , 2014

TFF yashauriwa kuipatia michezo ya kujipima nguvu timu ya taifa stars katika kipindi hiki ikiwa katika maandalizi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za africa AFCON 2015 michuano itakayofanyika nchini Morocco

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kinachotaraji kuingia kambini june 11 mwaka huu.

Wakati kikosi cha Taifa Stars kikitaraji kuingia tena kambini Jumatano Juni 11 mwaka huu kwaajili ya maandalizi ya mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam

Aliyekua kipa namba moja wa zamani wa timu hiyo Peter Manyika ya ametoa ushauri kwa TFF kuipatia stars mchezo mmoja wa kirafiki na moja ya timu ngumu iliyokatika nafasi za juu katika ubora wa viwango vya FIFA

Manyika amesema hata yakifanyika mazoezi ya aina gani kwa muda mrefu bila mechi ya kujipima uwezo tena na timu iliyojuu yetu katika ubora wa soka ni sawa na mwanafunzi kusoma bila kufanya mtihani kwa hiyo ni wazi hatutafika kokote kwa stahili ya kuogopa mechi na timu kubwa kwakua eti tutafungwa

Manyika amesema ni bora kufungwa na kujua mapunguvu kuliko kucheza na timu dhaifu na kuifunga kisha mkajua mko vizuri alafu baadae timu ikiingia katika mashindano inatolewa.