Alhamisi , 26th Dec , 2019

Uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya huenda ukawa sababu ya kuongeza kwa viporo kwenye ligi kuu soka Tanzania bara baada ya eneo la kuchezea 'pitch' kuharibika.

Muonekano wa eneo la kuchezea katika uwanja wa Sokoine Mbeya

Uwanja huo umeharibika kutokana na kufanyika kwa tamasha la muziki usiku wa kuamkia leo hivyo kufanya eneo la kuchezea kutokuwa rafiki kutokana na kuwa na tope jingi.

Mchezo wa ligi kuu unaotakiwa kuchezwa hapo kesho ni kati ya wenyeji Tanzania Prisons dhidi ya Yanga.

Muda huu tayari viongozi wa timu zote mbili wapo kwenye kikao ili kujadili muafaka wa mchezo huo. Pia viongozi hao wamekaa na wamiliki wa uwanja huo ambao ni CCM mkoa wa Mbeya.