Jumanne , 16th Jun , 2020

Meneja wa wachezaji Mohammed Ibrahim na Paul Bukaba ajulikanae kama Jamal Kasongo ametaja sababu za nyota hao kuchelewa kujiunga na timu ya Namungo ni kutolipwa mishahara yao tangu mwezi Februari.

Mo Ibrahim na wachezaji wengine wa Namungo FC

Wiki iliyopita uongozi wa Namungo ulitangaza mbele ya vyombo vya Habari kuwa imeachana wachezaji hao kutokana na utovu wa nidhamu kitu ambacho Kasongo amekikanusha vikali.

Kasongo amesema Namungo ilistahili kukaa kimya kwakuwa wao ndio walipaswa kuwapa wachezaji stahiki zao lakini hawakufanya hivyo badala yake wamekimbilia kwenye vyombo vya Habari kuwachafua wateja wake.

Kasongo amesema kitendo cha Namungo kutangaza kuwa imewaacha wachezaji hao ni makosa makubwa kwakuwa sio mali yao ni mali ya Simba ingawa mikataba yao inakaribia mwishoni.

Meneja huyo ameongeza kuwa Mo Ibrahim aliutaka uongozi wa Namungo kumpa pesa ili aiachie familia yake pamoja na kununua viatu lakini hawakumpa wakimtaka asafiri hadi Lindi ndipo watampa kiasi hicho.

Kwa upande wa Bukaba, Kasongo amesema mlinzi huyo yupo kwao Ukerewe jijini Mwanza hivyo bila kutumiwa nauli asingeweza kusafiri hadi Lindi kujiunga na timu hivyo anashangaa kuona wateja wake wakishafuliwa.