Jumapili , 19th Jun , 2016

Rekodi mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka na kuzifikia na kuzivunja katika klabu ya Catalunya FC Barcelona mshambuliaji raia wa Argentina Lionel Messi ameanza kufanya yake ndani ya kikosi cha nchi yake kinachoshiriki michuano ya Copa America

Lionel Messi akishangilia bao lake alilowafunga Venezuela hii leo.

Pamoja na magoli safi mawili ya kipindi cha kwanza ya mshambuliaji mwenye kasi Gonzalo Higuain nakuipeleka katika hatua ya nusu fainali Argentina baada ya kuiduwaza Venezuela bado nyota wa mchezo huo anabaki kuwa ni mshambuliaji mwenye kipaji cha hali ya juu Lionel Messi ambaye alifanya mambo makubwa ikiwemo kutengeneza mabao na pia yeye mwenyewe kufunga bao la rekodi.

Messi alithibitisha ustaa wake katika mchezo huodhidi ya Venezuela nakuiwezesha Argentina kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-1 mbapo sasa Waargentina hao watavaana na wenyeji Marekani katika nusu fainali itakayopigwa juma lijalo mjini Houston.

Goli moja alilofunga Lionel Messi katika mchezo huo kunako dakika ya 60 limemfanya mshambulaji huyo anayetumia zaidi mguu wa kushoto kufikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta ambaye alikuwa na rekodi ya mabao 54.
 
Ingawa mchango wake ulionekana ndani ya dakika nane mshambuliaji huyo alitengeneza [asisti] kwa mshambualiaji Higuain, amabye katika mchezo huo alicheza vema na kwakujiamini akiwa na msimu mzuri zaidi ndani ya klabu ya seria A Napoli.

Messi anaendelea kupigana ili kuiwezesha nchi yake na yeye pia kuwa wa kwanza na kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo maalumu ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza.

Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916.

Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.

Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.

Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.