
Staa wa Potland Trail Blazers, Damian Lillard akionyesha umwamba wake katika NBA.
Los Angeles Lakers ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Potland Trail Blazers kwa alama 100-93 mchezo ambao wa ukanda wa magharibi.
Damian Lillard alifunga point 34,CJ McCollum alifunga point 21,Jusuf Nurkik alifunga point 16 na rebounds 15 ,Camello Antony alichangia alama 11 na rebounds 10 hivyo kuiwezesha Blazers kuanza vyema kwenye mfululizo wa mchezo huo wa mtoano dhidi ya LA Lakers.
Kwa upande wa Lakers nyota wake Antony Davies alifunga points 28, rebound 11, Lebron James points 23, assists 16 na Kyle Kuzma akifunga point 14.
Huston Rockets walishinda kwa alama 123 kwa 108 za Oklahoma City Thunder ,huku James Harden akifunga point 37 na reboubd 11.
Miami Heat iliifunga Indiana Pacers 113 -101 ,Orlando Magic iliilaza Milwauke Bucks 122-110 na licha ya Bucks kupoteza,nyota wake Giannis Antetokounmpo alifunga points 31,rebounds 17 na assists 7.