Jumatano , 4th Nov , 2020

Raundi ya 10 ligi kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa michezo 3, Jijini Dar es salaam, Mkoani Lindi na Shinyanga, micheo yote inachezwa Saa 10:00 Jioni.

Baadhi ya matukio katika mchezo wa VPL kati ya Kagera Sugar na Simba .

Mabingwa watetezi Simba SC wanawakaribisha wanankurukumbi, Kagera Sugar mchezo utakao chezwa uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Msimu ulipota Simba walishinda michezo yote 2 ya ligi dhidi ya kagera na mchezo, ingawa katika michezo 5 ya mwisho timu hizi kukutana Kagera sugar wameshinda michezo 3 simba wameshinda 2 na wametosa sare mchezo 1.

Simba SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu kwenye michezo yao 3 ya mwisho (wamefungwa 2 wameshinda 1).

Ushindi wa bao 2-1 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar ndio ushindi pekee wa kagera kwenye michezo yao 5 ya mwisho (wamefungwa michezo 3 sare 1).

Tofauti ya timu hizi kwenye msimamo wa ligi ni alama 8, mabingwa watetezi Simba wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 16 wakati Kagera wana alama 8 wanashika nafasi ya 16.

Huko kusini mkoani Lindi, Namungo FC watamenyana na JKT Tanzania katika dimba la Majaliwa, timu zote hazijawa na msimu mzuri mpaka sasa, hususani Namungo ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Namungo imeshinda michezo 4 tu kwenye michezo 9 ya ligi iliyocheza mpaka sasa, wamefungwa michezo 4 na wametoka sare mchezo 1, wamekusanya alama 13 na wapo nafasi ya 8 kwenye msimamo.

JKT Tanzania ipo nafasi ya 13 wakiwa na alama 9 katika michezo 9 ya ligi na ni timu ya pili iliyoruhusu mabao mengi ambapo wameruhusu mabao 12 wakiwa nyuma ya mwadui waliofungwa mabao 19 mpaka sasa.

Msimu uliopita Namungo ilishinda michezo yote miwili ya ligi kwa ushidi unaofanana wa bao 1-0.

Baada ya vipigo vizito mfululizo vya bao 6-1 kutoka kwa JKT Tanzania na cha bao 5-0 kutoka kwa Simba SC, Klabu ya Mwadui itakuwa inajiuliza mbele ya Ruvu shooting kwenye uwanja wao wa nyumbani wa (Mwadui complex) mkoani Shinyanga.

Ruvu shooting chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa 'Master' ipo kwenye mwendelezo bora wa matokeo, hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo 4 ya mwisho, wameshinda michezo 3 ukiwemo ushindi dhidi ya mabingwa watetezi Simba SC na wametosa sare mchezo 1.

Ruvu walichukua alama 4 dhidi ya mwadui msimu uliopita walishinda mchezo mmoja 3-2 na mwingine ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Mwadui wapo nafasi ya 15 wana alama 9, Ruvu shooting wana alama 15 wapo nafasi ya 6.