
Mshambuliaji kinara wa Simba, Meddie Kagere ambaye ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting
Vinara wa ligi Azam FC wapo mkoani Morogoro wataminyana na wenyeji wao Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri.
Mtibwa wameshinda mchezo uliopita dhidi ya Namungo kwa goli 1-0 na ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Mtibwa baada ya kupoteza michezo 3 mfululizo.
Azam hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo yote 7 na ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 2.
Katika michezo 2 ya ligi msimu uliopita Mtibwa walishinda mchezo 1 kwa goli 1-0 na mchezo mwingine ulimalizika kwa sare ya goli 1-1.
Uwanja wa Uhuru Dar es salaam mabingwa watetezi Simba SC baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa goli 1-0, jioni ya leo wana waalika Ruvu shootung ya Pwani.
Simba walichukua alama 4 dhidi ya Ruvu kwenye michezo ya ligi msimu uliopita ambapo walishinda bao 3-0 mchezo wa kwanza na wa pili ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu hizi zinatofautiana alama 3 tu kwenye msimamo wa ligi, Simba wana alama 13 kwenye michezo 6 wapo nafasi ya 4, wakati Ruvu shooting wana alama 9 katika michezo 7 na wapo nafasi ya 11.
Mchezo mwingine utachezwa mkoani Iringa uwanja wa Samora, Dodoma Jiji FC watachuana na Tanzania Prisons.
Dodoma FC wanautumia uwanja wa Samora Iringa kama uwanja wao wa nyumbani kufuatia uwanja wa Jamhuri kufungwa kupisha matengenezo.
Kikosi cha kocha Mbwana Makata, Dodoma FC wana alama 12 katika michezo 7 na wameshinda michezo 3, sare michezo 3 na wamefungwa mchezo 1 wapo nafasi ya 5, na wemetoka sare katika michezo 2 mfululizo iliyopita,
Tanzania Prisons wataingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Simba SC bao 1-0 kwenye mchezo uliopita.
Usindi huo kwa Prisons ulikuwa ni ushindi ni wa pili msimu huu katika michezo 7,lakini wamefungwa michezo 2 na sare michezo 3 wana alama 9 wapo nafasi ya 9.