Jumanne , 17th Nov , 2020

Baraza la Michezo la Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kuwa yatafanyika katika vituo viwili vya Arusha na Karatu na kuanzia Novemba 22 hadi Disemba 2.

Rais wa CECAFA, Wallace Karia(Pichani) akizungumzia matayarisho ya mashindano ya vijana yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Rais wa CECAFA, Wallace Karia amesema amesema michuano hiyo ilikuwa ifanyike Aprili mwaka huu nchini Sudan lakini kutokana na kuibuka na homa ya mafua ya Corona (COVID 19) ikabidi kuahirishwa na ndio yatafanyika mwishoni mwa wiki hii.

''Kuwa kuwa kwa taratibu zilizotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu barani African CAF juu ya kuzingatia kanuni za ungonjwa wa Covid 19,mechi zote hazitakuwa na mashabiki na pia watafata miongozo ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo wachezaji kupimwa kila baada ya masaa 48'' amesema Rais Wallace Karia.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidao amesema michuano hiyo imepangwa katika makundi matatu ambapo timu zitakazo ongonza makundi zitaingia moja kwa moja nusu fainali huku moja ikipita kwa best loser.

'' Maandalizi yamekamilika kwa upande wao kama wenyeji wa mashindani ,hasa katika kuboresha miundombinu ya viwanja vya kucheza mechi na viwanja vya mazoezi,hotel kwaajili ya timu zote na viongozi wa CAF na CECAFA tayari wamepangalia vizuri'' amesema katibu Wilfred Kidao,

Timu zitakazo shiriki ni wenyeji Tanzania, Zanzibar, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini huku Eritrea na Rwanda ndio pekee ambao hawata shiriki.