Jumatano , 16th Jun , 2021

Mshambuliaji mahiri wa Austria Mark Arnautovic amefungiwa kucheza mechi 1 ya kundi C katika mashindano ya EURO2020 yanayoendelea kwa sasa Ulaya kufuatia kitendo chake cha kutoa lugha ya ubaguzi kwa akina Mama wa Albania.

Mark Aurnatovic

Arnautovic alifanya tukio hilo wakati anashangiilia goli alilofunga dhidi ya Marcedonia ya Kaskazini katika mchezo wao wa kwanza wa mashindano hayo walipoibuka na ushindi wa mabao 3-1, ambapo yeye alifunga goli la 3.

Austria ipo kundi C pamoja na Uholanzi, Ukraine na Marcedonia kaskazini,ambao wao ndiyo wanaongoza kundi hilo , kutokana na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa kufuatia ushindi wa bao 3-1.

Arnautovic nyota wa zamani wa West ham ya Uingereza iwapo atakosekana katika mechi ijayo dhidi ya Uholanzi hapo kesho ni wazi atapunguza nguvu kubwa sana katika timu hiyo inayomtengemea sana yeye na nahodha wao David Alaba aliyejiunga na Real Madrid akitokea Bayern Munich kwa msimu ujao.