
Juu ni Simba na chini ni Mtibwa Sugar
Ninje amesema ana imani na vilabu hivyo kuwa vimejiandaa vya kutosha na wao kama TFF wanaamini mechi zao za ugenini zitakuwa za kiungwana na watafuatilia kila hatua kuhakikisha vilabu vyao vinatendewa haki.
''Tunaamini wachezaji wana uzoefu na watafuata kile walimu watakachowaambia na hawataathiriwa na mambo ya nje ya uwanja kama ambavyo huwa inatokea kwenye mechi nyingi za ugenini'', amesema Ninje.
Aidha Ninje amesisitiza kuwa shirikisho linaamini katika 'Fair Play' na dunia ya soka inataka hivyo kwahiyo Simba na Mtibwa hawatakiwi kuyumbishwa na propaganda za nje ya uwanja.
Simba leo watakuwa jijini Manzini, eSwatini kukipiga na wenyeji wao Mbabane Swallows wakati Mtibwa Sugar wao wapo jijini Victoria huko Seychelles ambapo kesho watakipiga na wenyeji wao Northen Dynamo.