Jumanne , 14th Jul , 2015

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amemualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete katika mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema, anamuomba Kikwete kuhudhuria mechi hiyo itakayochezwa Septemba tano uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ili kuondoa dhana ya kusema kila akija uwanjani timu ya Taifa inafungwa.

Mkwasa amesema, wanaamini watafanya vizuri katika mechi hiyo na wanaamini kutokana na maandalizi yaliyopo katika timu hiyo, Kikwete ataanza upya kuhudhuria mechi za timu ya taifa.