Jumamosi , 8th Aug , 2020

Aliyekua nyota wa Klabu ya Yanga, Benard Morrison amesaini Mkataba wa kuitumikia miamba ya soka nchini Tanzania, wekundu wa Msimbazi Simba.

Winga Machachari ,Benard Morrison akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Klabu ya Simba.

Nyota huyo ambaye alitikisa vilivyo tangu kufanyika kwa usajili wake , aliripotiwa kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Yanga, lakini yeye alikanusha kuwa mkataba wake ungemalizika kati kati mwa mwezi Julai .

Uongozi wa Yanga , kupitia makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hersi Said alisema ''

“ Morrison alisaini mkataba wa miaka miwili mbele ya macho yangu ambao upo TFF na FIFA . Baada ya muda alikuja kuomba kuvunja mkataba huo kwa kuwa kapata timu yenye masilahi zaidi kwake .

Tuliligomea hilo kwa kuitaka hiyo klabu ije mezani kama klabu kusikiliza ofa yetu sio yeye . Hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu ya Yanga . Wanaomvuruga Morrison waje tu mezani wapewe ofa yetu tutamuuza bila shida “ Engineer Hersi Said.