
Haji Manara na Masau Bwire
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa hataki kufananishwa na msemaji yoyote kwani hakuna anayefanana naye na hata akiingia ulingoni na mtu anaua.
"Kwani huyo Masau Bwire ndio nani?. Please sitaki kesi zisizo na fedha, hawa watu waambieni mimi kila asubuhi nakunywa supu ya damu ya fisi jike na kongoro la paka shume, Ohooooooo", ameandika Manara.
"Yeye anataka kupigana ulingoni na mimi kwanza ana kilo ngapi?, anakula mara ngapi kwa siku?, mimi nikipigana naua, kwanza yeye anasemea mpira huu ninaoujua mimi?, maana najua msemaji ni mmoja tu", amesema.
Haji Manara na Masau Bwire wamekuwa na mikwaruzano mara kwa mara wanapokuwa wanazisemea timu zao, kila mmoja akijinadi kuwa ni bora kuliko mwenzake.