Alhamisi , 28th Mei , 2020

Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa klabu hiyo ndiyo ya kwanza kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko tofauti na watu wengi wanavyofikiria.

Antonio Nugaz

Akizungumza katika kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio, Nugaz amesema kuwa Yanga ilianza mpango wa mabadiliko tangu mwaka 2010 huku msimamizi wa mchakato huo akiwa ni Wakili Alex Mgongolwa ambaye yupo mpaka sasa kwenye mchakato unaoendelea.

"Watambue kuwa Yanga ilianza mabadiliko tangu 2010 na haikushindikana bali iliishia kwenye hatua ya kwanza. Sisi hatuna haja ya kuanzisha Yanga kampuni sijui na vitu gani kwa sababu hivyo vyote vilishafanyika nyuma", amesema Nugaz.

"Huyu Alex Mgongolwa mnayemuona alijuwepo tangu mwanzo kwahiyo tunaanza tulipoishia. Pia mtambue kuwa Yanga itabakia kuwa Yanga ila mfumo wa uendeshaji wa klabu ndioo utabadilika", ameongeza.

Mtazame zaidi hapa akizungumza zaidi.