
Katibu Mkuu wa Mtwarefa Charles George amesema, Kocha Malale aliombwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ kupitia Chama cha Soka visiwani Zanzibar ZFA na anaendelea na majukumu yake na JKU mpaka hapo watakapomaliza mechi za kimataifa ambapo hawajajua Malale atakuwa visiwani humo kwa muda gani kutokana na timu ya JKU kusonga mbele katika michuano hiyo.
George amesema, timu ipo chini ya kocha msaidizi na hivyo wanajitahidi kupata kocha mwingine wa kumuongezea nguvu ili timu ya Ndanda FC iendelee kubaki sehemu salama katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
George amesema, Kocha atakayekuja atakuwa wa muda hivyo kocha Malale atakaporudi nafasi yake itakuwepo kwani bado ana mkataba wa miaka miwili na Ndanda FC hivyo ataendelea na mkataba wake na walikubaliana kipindi ambacho hatokuwepo mkataba wake pia utasimama kwa kuwa atakuwa anaitumikia sehemu nyingine.