Alhamisi , 26th Feb , 2015

Nahodha wa Timu ya Taifa ya wanawake, Sophia Mwasikili amesema wachezaji wa kike wanakosa nafasi za kucheza soka la kulipwa zinakuwa ngumu kutokana na kutokuwa na mshindano ya kutosha kwa timu za wanawake hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwasikili amesema, iwapo kutakuwa na mechi za kirafiki itasaidia kwani mchezaji anapotaka kucheza soka la nje anatakiwa kuwa na rekodi ambayo itakuonesha anachofanya katika timu yake au timu yake ipo vipi katika mechi mbalimbali.

Mwasikili amesema, mchezaji kutoka ni kama awe na jina kubwa lakini katika kuwa na rekodi ni ngumu kwasababu wachezaji hawaonekani kutokana na kutokuwa na Ligi mbalimbali pamoja na mechi za kirafiki ambazo zinasaidia kujua kipaji alichonacho mchezaji.