Nyota wa tennis Rafael Nadal
Nadal mwenye umri wa miaka 36 alimshinda Kudla kwa seti 6-3 na 6-2 na kufikisha michezo 11 kushinda kwenye michezo yote aliyoshiriki msimu huu huku akijivunia rekodi aliyowekwa mwezi uliopita wa kutwaa ubingwa wa 21 wa Grand Slam mjini Melbourne.
Kwingineko nyota anayekamata nafasi ya pili kwa viwango vya ubora duniani Mrusi Daniil Medvedev baada ya kuchapwa kwenye fainali ya Australian 2022 dhidi ya Rafael Nadal yeye alichomoza na ushindi wa seti 2-0 ( 6-3 ,6-4) dhidi ya Mfaransa Benoit Paire huku wiki ijayo akitarajiwa kucheza na Mhispainia Pablo Andujar huku Medvedev anaweza kushika nafasi ya kwanza iwapo Novak Djokovic atafanya vibaya kwenye michuano anayoshiriki mjini Dubai.
Upande wa wanawake kwenye michuano ya wazi ya Jalisco maarufu kama Guadalajara Open ,bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya Marekani ,Muingereza Emma Raducanu ameondoshwa katika mzunguko wa kwanza baada ya kupata maumivu ya paja na kushindwa kuendelea mbele ya Muaustralia Daria Saville aliyepata ushindi wa seti 5-7 7-6 (7-4) 4-3 .


