Nahodha wa Yanga aachwa

Alhamisi , 14th Mar , 2019

Klabu ya soka ya Yanga imeondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Iringa kwenye mchezo wake wa Ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Lipuli FC huku ikimuacha nahodha wake msaidizi Juma Abdul.

Kikosi cha Yanga

Daktari wa timu hiyo Dr. Bavu ameeleza kuwa kikosi chake kina majeruhi wawili ambao ni nahodha msaidizi na Juma Abdul pamoja na Vicent Andrew.

''Timu imesafiri bila Juma Abdul ambaye ni majeruhai lakini Andrew Vicent amesafiri na anaweza kucheza au asicheze kwasababu aliumia kwenye mchezo dhidi ya KMC lakini anaendelea vizuri'', amesema Bavu.

Mbali na hao, nyota mwingine ambaye atakosa mchezo huo ni Abdallah Shaibu ambaye anaanza kutumikia adhabu yake ya michezo mitatu aliyofungiwa na shirikisho la soka nchini FIFA kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union.

Yanga ina alama 67 kwa michezo 27 inaongoza ligi huku Lipuli ikishika nafasi ya 5 kwa alama 39 walizokusanya katika michezo 30.