
Wachezaji wa Namungo FC
Kocha mkuu wa kikosi cha Namungo Hemed Morocco amesema malengo kueleka mchezo huu dhidi ya Pyramids ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi lakini wanajua wanacheza na timu kubwa, “Tunaiheshimu Pyramids, ni timu kubwa. Tunaenda kuikabili tukiwa na malengo ya kupata alama tatu. Hautakuwa mchezo rahisi ila tuko tayari”, amesema kocha Morocco.
Namungo FC walipoteza mchezo wa kwanza wakundi hili kwa kufungwa bao 1-0, wakiwa ugenini dhidi ya Raja Casablanka ya Morocco hivyo hii leo watakuwa na kibarua cha kuhakikisha wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani, Pyramids wao walishinda mchezo wa kwanza kwa kuifunga Nkana ya Zambia mabao 3-0 na ndio vinara wa kundi hilo.
Mchezo huu ambao ni wa kihistoria kwa klabu ya Namungo FC kwani hii ni mara ya kwanzo kikosi hicho kutoka kusini mwa Tanzania kushiriki mashindano haya na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi, mchezo huu unachezwa majaira ya Saa 10:00 jioni uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.