Jumatano , 17th Mar , 2021

Mshambuliaji wa Real Madrid raia wa Ufaransa Karim Benzema, amekuwa mchezaji wa tano kufikisha mabao 70 kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, mshambuliaji huyo alifunga goli 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 walioupata dhidi ya Atalanta jana usiku.

Karim Benzema

Goli la jana lilikuwa la 5 kwa Benzema msimu huu kwenye michuano hiyo ya ligi ya mabaingwa, na linamfanya awe mchezaji watano kufikisha mabao 70 kwenye historia ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya, anaungana na kinara wa ufungaji wa muda wote Cristiano Ronaldo mwenye mabao 134, Lionel Messi mwenye mabao 120, Robert Lewandowsk mabao 72 na msahambuliaji wa zamani wa Real Madrid Raul Gonzalez mwenye mabao 71.

Pia bao hilo ni la 21 kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, katika michuano yote akiwa amecheza jumla ya michezo 31 msimu huu, na anamzidi mchezaji anaefata kwa tofauti ya mabao 15 kwenye orodha ya wafungaji wa Real Madrid msimu huu.

Mabao mengine ya Madrid usiku wa jana yalifungwa na Sergio Ramos kwa mkwaju wa penati na Marco Asensio, wakati lile la Atalanta lilifungwa na Luis Muriel, na ushindi huu umeifanya Real Madrid kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 2018.