Alhamisi , 22nd Oct , 2020

Kocha mkuu wa timu ya Arsenal Mikel Arteta, amekiri kuhusika moja kwa moja na kumuondoa Mesut Ozil katika orodha ya wachezaji watakao cheza ligi kuu ya England na mashindano ya Ulaya kwa msimu wa 2020/2021

Mikel Arteta na Mesut Ozil wakipongezana katika moja ya mechi za Arsenal,wakati Arteta akiwa bado anacheza

Arteta alisema “Kila moja ana uhuru wake wa kutoa mawazo yake juu ya suala Ozil, lakini ukweli maamuzi yangu ni ya kiufundi zaidi, hakuna uhusiano na mambo ya kisasi wala kisirani cha jambo lolote la Ozil la siku za nyuma, Ozil amepoteza uwezo wa kuipambania timu''

Kuondolewa kwa Ozil katika kikosi kitakacho shiriki mashindano, mawili tofauti ikiwemo ligi kuu na mashindano ya Ulaya, kumezusha maswali mengi juu ya yake, ndiyo maana kocha Arteta akalazimika kuweka wazi sababu za kuondolewa kikosini

Wadadisi wa mambo wanahusisha matatizo ya Ozil na mtizamo wa kisiasa, wapo wanaohusisha na mtizamo wa kiimani kuna wakati fulani Ozil alitoa maoni yake juu ya imani ya dini mojawapo kwa watu wa China, wapo wanaohusisha na suala la kimaslahi ndani ya Arsenal ikiwemo kukataa kukatwa mshahara wake wakati wa janga la Corona

Kwa sasa Ozil hana nafasi ya kuichezea Arsenal katika mechi za kimashindano hadi dirisha dogo la mwezi Januari endapo Arteta atahitaji kumjumuisha kikosini